Amos 6:4-7


4 aNinyi mnalala juu ya vitanda vilivyofunikwa kwa pembe za ndovu,
na kujinyoosha juu ya viti vya fahari.
Mnajilisha kwa wana-kondoo wazuri
na ndama walionenepeshwa.

5 bNinyi mnapiga vinubi kama Daudi,
huku mkitunga nyimbo za vinanda mbalimbali.

6 cMnakunywa mvinyo kwa bakuli zilizojazwa,
na mnajipaka mafuta mazuri,
lakini hamhuzuniki kwa maangamizi ya Yusufu.

7 Kwa hiyo mtakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kwenda uhamishoni;
karamu zenu na kustarehe kutakoma.

Bwana Anachukia Kiburi Cha Israeli

Copyright information for SwhKC